Baadhi
ya walimu wa shule za msingi na sekondari wa Halmashauri ya
Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa
shule ya msingi Itigireli wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CWT.
Katibu
wa idara ya Utumishi wa walimu(TSD) Mkoa wa Singida,Bwana Ole
Saitabau(anayeandika mahudhurio katika kitabu) na kulia kwake ni kaimu
afisa elimu Mkoa wa Singida.
Naibu
katibu Mkuu wa CWT,Bwana Eliezer Oluoch akizungumza na walimu wa shule
za msingi na sekondari wa Halmashauri ya Itigi.(Picha zote Na Jumbe
Ismailly)
Ni Majengo ya ofisi za muda za Halmashauri ya Itigi
Na Jumbe
Ismailly,Itigi
WILAYA
ya Manyoni,Mkoani Singida inaongoza Mkoani hapa kwa kushindwa kushughulikia
kero zinazowakabili walimu wa wilaya hiyo,na hivyo kusababisha malalamiko
yasiyofanyiwakazi kuongezeka siku hadi siku.
Hayo
yamebainishwa na walimu wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya
Itigi na Halmashauri ya wilaya ya Manyoni waliohudhuria katika kikao
kilichoandaliwa rasmi kuonana na Naibu katibu mkuu wa cwt alikuwa na ziara ya
siku moja wilayani Manyoni.
Wakizungumza
kwa hasira kali kutokana na matatizo yao wanayowasilisha kwa afisa utumishi wa
wilaya ya Manyoni na kwa katibu wa idara ya utumishi (TSD) wilaya hiyo,walimu
hao wameweka wazi kwamba imekuwa ni kawaida kwao kunyanyaswa na watendaji hao
wawili kila wanapokwenda kupeleka matatizo yao.
Mmoja
wa walimu hao ambaye pia ni mratibu elimu wa kata ya Tambukareli,katika
Halmashauri ya Itigi,Edsoni Nkinga alisema kwamba wamefurahia kusikia kati ya
Halmashauri zenye matatizo Manyoni inaongoza kwa kushindwa kusikiliza na
kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya walimu wa wilaya hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...