Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Chacha (katikati)akizungumza na wananchi juu ya kuwashukuru sana wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kwa kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho, Jiji la Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw.Freeman Mbowe akizungumza na wananchi  baada ya   ushindi wa kiti hicho cha meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 Wafuasi wa chadema wakingombania bendera mara baada ya uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Chacha akisindikizwa na wananchi wa  kuelekea Makao Mkuu ya Chama hicho,leo Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wafuasi wa Chadema  waliojitokeza katika uchaguzi huo, leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

KAIMU Mkurugenzi  Jiji  la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Isaya Chacha Diwani wa  Kata ya Vijibweni  (CHADEMA) kutoka Wilaya ya Temeke kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya Uchaguzi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema hayo mara baada ya uchaguzi uliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea mweza kupitia chama cha CCM Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67,na katika uchaguzi huo kura 7 ziliharibika.

 “Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kulifanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili”,alisema Bi Yohana.

Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa  Jiji Mhe. Chacha alisema anawashukuru sana wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kwa kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.

“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji pia hakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili katika kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.

Mbali na hayo naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha meya ni lazima uchukuliwe na  CHADEMA sababu  madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...