Mwanzilishi wa Bites& Bytes, Lilian Madeje (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano la kiteknoloJia litakalofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na  jijini Dar es Salaam Machi 29 ,30 Machi 31 utafanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa utafiti  wa FSDT(Financial Sector Deepening Trust) , Elvis Mushi.
   (Head of New business venture),Eric Luyangi (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kutoka kushoto ni Senior advisor ,communication Twaweza, Risha Chande, Mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje na wamwisho kulia mwakilishi wa FSDT , Elvis Mushi.

ASASI isiyo ya kiraia ya Twaweza, CBA,FSDT,TWAWEZA na IBM ikishirikiana na Bites &Bytes imeandaa mkutano mkubwa wa Kiteknolojia na uvumbuzi unaoitwa Bites &Bytes ambao utafanyika Machi 29 30  mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Mahi31 utakuwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Liliani amesema kuwa lengo mkutano huo ni kuhamasisha uendelezaji wa mawazo mpya pamoja na uvumbuzi wa mawazo mapya ya kibiashara ili aanzishaji wapya wa mawazo waweze kuwapa mwanya wa kubadilishana mawazo na wadau wengine ili waweze kushirikiana kwa pamoja.

Pia Liliani amesema kuwa washiriki 16 wa mechanguliwa kushiriki katika shindano hilo la ubunifu wa biashara ambapo washiriki hao watashindania kuwania kitika cha shilingi milioni tano(5,000,000).

Nae  (Head of New business venture), Eric Luyangi amesema kuwa katika shindano hilo la Software Developers wanalenga kuleta suluhisho la kuwezesha kufikisha takwimu na tafiti mbalimbali za Twaweza kwa kutumia mitandao tofauti tofauti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...