Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuujulisha umma
kuwa kivuko cha MV Kilombero II ambacho kilizama tarehe 27 Januari
2016, na kusababisha kusimama kwa hudum ya kivuko kwenye Mto
Kilombero Mkoani Morogoro kimeanza kufanyakazi rasmi tarehe 29
Februari, 2016 mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Kivuko hicho kinaendelea na ratiba yake ya utoaji huduma ya kivuko
kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 1:00 jioni kama kawaida.
Wizara inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza wakati kivuko
hicho kikiwa kwenye matengenezo.
Taarifa hii imetolewa na,
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI),
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
02 Machi, 2016


Hii picha ya gari iliyokuwa kwenye kivuko mbona inatishia usalama wa raia? Sidhani kama hayo magogo yamefungwa sawasawa,wala sioni kama dereva ameangalia usalama wa haya magogo na usalama wa binadamu.
ReplyDeleteTunaomba madereva na wadau wengine kuangalia suala la usalama kwanza ili kuepuka ajali.
Ni maoni yangu na mtazamo wangu tu...