Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye ametoa agizo rasmi juu ya matumizi ya tiketi za Kielekroniki michezoni kwa kulitaka Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuakikisha linatumia tiketi hizo kuanzia Machi 9.2016 na kuachana na tiketi za kawaida huku akibainisha kuwa wataendelea kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu na hatua zaidi ilikuziba mianya ya udanganyifu.

Nape amebainishahayo muda huu wakati anazungumza na vyombo vya habari kuelezea suala la Michezo hapa nchini ikiwemo suala hilo la mfumo wa malipo kwa njia ya Kielekroniki ambapo awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo la matumizi ya mfumo huo.Akielezea suala hilo, amesema litaondoa ‘figisufigsu’ za mara kwa mara ambazo watu wamekuwa wakilalamikia mapato ikiwemo hayo ya Uwanja wa Taifa.

“Baada ya Machi 8 mwaka huu. Mechi zote zitakazochezwa uwanja wa Taifa, tiketi zote zitatumika ni zile za kieletroniki. Hii ni mara baada ya michezo yote mitatu iliyobaki ambayo TFF wanamalizia tiketi zao ambazo wamebazibakisha na zinaisha Machi 8. Safari hii tutafuatilia na kukagua wenyewe. Hatutakubali kuendelea kuvumilia hujuma katika hili.” Ameeleza Nape katika mkutano huo.
Nape
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (Kulia) akizungumza na mwanahabari (Hawapo pichani) wakati akitoa tamko hilo muda huu juu ya kuitaka TFF, kuakikisha inatumia mfumo wa malipo ya Kielekroniki kuanzia Machi 9 na kuendelea kwa michezo yote ndani ya Uwanja wa Taifa huku akielezea kuwa wataendelea kufuatilia ilikubaini udanganyifu zaidi katika suala la mapato la milangoni katika michezo yote. (Picha na Andrew Chale).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wapi alipo mpongeza cheka? uandishi wa dotcom, shaghalabagala!

    ReplyDelete
  2. Wanahabari wa bongo??
    mmmh haya ...hayo ndiyo maelezo ya serikali kumpongeza Cheka??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...