Michezo saba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuchezwa katikati ya wiki hii, kwa kesho kuchezwa mchezo mmoja, huku michezo mingine sita ikichezwa siku za Jumatano na Alhamisi katika viwanja mbalimbali nchini.
Kesho Jumanne, Young Africans watakua wenyeji wa Wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaoanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Jumatano Machi 09, 2016 Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Coastal Union wakicheza na ndugu zao maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mwadui FC watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Toto African katika uwanja wa Mabatini , Mlandizi mkoa wa Pwani.
Alhamisi Simba SC watawakaribisha Ndanda FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City wakiwakaribisha Stand United chama la wana katika uwanja wa Sokoine.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...