Na Zuena Msuya
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amepokea ripoti
maalumu ya kumaliza mgogoro wa wananchi wa Nyamongo na mgodi wa
wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia North Mara uliodumu kwa miaka 6
sasa.
Akizungumza mjini Tarime Mkoani Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Prof.
Muhongo ameshauri wananchi wa Tarime kuwa watulivu wakati akiendelea
kuisoma ripoti hiyo na kutolea majibu mambo yalioyo andikwa katika riporti
hiyo.
Profesa Muhongo alisema anaimani mambo yote yalioandikwa katika ripoti
hiyo ni mawazo ya wananchi waliohojiwa na atashangaa endapo kuna mtu
atajitokeza kuikataa.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya Tarime,Glorious Luoga alisema ripoti
hiyo itatoa majibu stahiki kwa wanaohitaji kulipwa na hata wasiostahili
hivyo wananchi wakae tayari kupokea utekelezaji wa ripoti baada ya
kusoma na kupitishwa na Waziri.
Naye Mbunge wa Tarime vijijini John Heche alisema kuwa anaimani na
ripoti hiyo kuwa itatenda haki kwa wananchi wake wa Nyamongo ili
kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati akiomba kura kuwa hatamaliza
kabisa tatizo la Nyamongo lililodumu kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi John Nayopa alisema kamati hiyo
imepokea malalamiko zaidi ya 4400 ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka
mgodi,malalamiko ambayo yalilenga masuala ya fidia ya ardhi,athari za
shughuli za mgodi hasa upande wa mazingira,uvamizi wa mgodi,sakata la
tegesha na Askari kutuhumiwa na kunyanyasa na kutesa wananchi.
Kamati hiyo iliundwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo mwezi mmoja uliopita ina wajumbe 27,19 wataaalamu wa
Serikali, na Wenyeviti wa vitongoji 80.
Mwenyeki wa kamati John Nayopa akimkabidhi Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo,Taarifa ya kamati ya kushughulikia
mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Nyamongo
na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,akionesha taarifa
aliyokabidhiwa na Kamati hiyo ambapo ameahidi kuisoma na kuitolea
majibu yanayostahili ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu Machi 23,2016
alipokabidhiwa taarifa hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza
jambo mara baada ya kupokea Taarifa ya utekelezaji kutoka kwa
Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji
vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani
Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa
North Mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...