JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
![]() |
.
|
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa
familia ya Balozi Joseph Rwegasira, aliyefariki dunia jana tarehe 04 Machi,
2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Balozi Joseph
Rwegasira amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Wakati wa uhai
wake, Balozi Rwegasira amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini zikiwemo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Balozi wa Tanzania nchini
Zambia.
Katika salamu zake
kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Rais Magufuli amesema Taifa litaukumbuka mchango mkubwa uliotolewa
na Marehemu Balozi Rwegasira katika harakati za kukuza diplomasia na kuleta
amani katika nchini majirani.
Rais Magufuli ameongeza
kuwa Marehemu Balozi Rwegasira alikuwa mchapakazi, muadilifu na mzalendo wake
kweli kwa nchi yake.
"Tungependa
kuendelea kumuona Marehemu Balozi Rwegasira akiwa hai, lakini siku zote kazi ya
Mungu haina makosa, namuombea kwa Mwenyezi Mungu apumzishwe mahali pema peponi,
Amina" Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli
amewataka familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kuwa wavumilivu na
wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba anaunga nao katika kumuombea
marehemu.
Bwana ametoa na
Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
05 Machi,
2016.



Angalia Kichwa cha habari nadhani kinahitaji marekebisho.
ReplyDelete''Mungu amlaze peponi'