JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Balozi Joseph Rwegasira, aliyefariki dunia jana tarehe 04 Machi, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Balozi Joseph Rwegasira amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Wakati wa uhai wake, Balozi Rwegasira amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini zikiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkuu wa Mkoa   wa Dar es Salaam na Balozi wa Tanzania nchini Zambia.

Katika salamu zake kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Rais Magufuli amesema Taifa litaukumbuka mchango mkubwa uliotolewa na Marehemu Balozi Rwegasira katika harakati za kukuza diplomasia na kuleta amani katika nchini majirani.

Rais Magufuli ameongeza kuwa Marehemu Balozi Rwegasira alikuwa mchapakazi, muadilifu na mzalendo wake kweli kwa nchi yake.
"Tungependa kuendelea kumuona Marehemu Balozi Rwegasira akiwa hai, lakini siku zote kazi ya Mungu haina makosa, namuombea kwa Mwenyezi Mungu apumzishwe mahali pema peponi, Amina" Amesema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amewataka familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba anaunga nao katika kumuombea marehemu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
05 Machi, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Angalia Kichwa cha habari nadhani kinahitaji marekebisho.
    ''Mungu amlaze peponi'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...