Serikali imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi hapa nchini.


Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika mapambano hayo.

Aidha, amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba maalum ya uzinduzi wa kongamano hilo 




Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia dozi hiyo.

Hata hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure kwa watumiaji wake.

Kongamano hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre – congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group. 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu ambao ni wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya Kisukari wakiwa tayari kutoa ujumbe kwa Serikali kuona namna ya kusaidia jamiii katika mapambano ya ugonjwa wa kisukari.

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...