DIONICE ANATOLY MFINANGA (1984 – 2016)

Familia ya Bwana & Bibi Anatoly Henry Mfinanga wa Chanjale, Kisangara, Mwanga Kilimanjaro inapenda kutoa shukrani kwa watu mbalimbali walio fanikisha shughuli nzima ya mazishi ya ndugu yetu mpendwa DIONICE ANATOLY MFINANGA (32) aliye fariki  kwa kuuwawa na majambazi usiku wa kuamkia tarehe 06/02/2016 siku ya jumamosi maeneo ya Survey Dar es Salaam.

Shukrani zetu ziwafikie ndugu wote upande wa baba na mama hususani shukrani za kipekee ziwandee Baba Hashimu Kiure, Mjomba John Msami na Baba Halifa Katani kwa kutuongoza tangu siku ya tukio tarehe 06/02/2016 nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndg. Boniface A. Mfinanga Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam hadi siku ya kusafirisha mwili wa marehemu siku ya jumatatu tarehe 08/02/2016 kwenda nyumbani Chanjale, Kisangara, Mwanga, Kilimanjaro.

Shukrani ziwaendee pia wanamalezi wote wa Chanjale Seminary katika umoja wao kwa ushirikiano tangu kutoa taarifa ya kifo hadi siku ya mazishi, tunawashukuru Class mate wa marehemu MBA 2015 Mzumbe University kwa ushirikiano wao kupitia wawakilishi wao. Shukrani ziwaendee pia majirani wote wa marehemu wa Kimara Korogwe, wafanyakazi wa Ubalozi wa Afrika Kusini, Tanganyika Arms Ltd, jumuiya ya Mashahidi wa Uganda Rau parokia ya Moshi mjini, Jumuiya ya Mt.

 Petro Parokia ya Mwanga  kwa ushirikiano na michango yao.

Kadhalika tunapenda kuwashukuru majirani wote mbezi kwa Msuguri nyumbani kwa kaka wa marehemu kwa ushirikiano wao wote wa hali na mali waliouonyesha.

Tunatoa shukrani zetu pia kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama mwajiri wa marehemu kwa ushirikiano wa hali na mali walio uonyesha kuanzia siku ya tukio hadi siku ya mazishi.

Shukrani za kipekee zimuendee Baba Askofu Jacob Venance Koda pamoja na Baba Poroko Samwel J. Lawena Parokia ya Chanjale na team yote ya mapadre kwa kutuongoza katika ibada ya kumsindikiza ndugu yetu Dionice katika nyumba yake ya milele. Shukrani pia ziwaendee majirani wote wa Mwanga na kijijini kwetu Chanjale Kisangara, Mwanga kwa umoja katika kufanikisha shughuli nzima za mazishi.

Tuanajua ni watu wengi waliojitolea kwa ajili ya kufanikisha shughuli nzima ya mazishi na msiba kwa ujumla hivyo kwa yeyote ambaye hatukumtaja hapa atuwie radhi ila tunathamini sana kile alichkitoa kwa ajili yetu. Kama familia hatuna la kuwalipa ila Mungu aliyewapa Moyo wa kujitolea awabariki sana.

 Zaidi ya shukrani hizo wote tunajua leo tarehe 6/3/2016 ni mwezi mmoja tangu mpendwa wetu Dionice atutoke ghafla, tumebaki na kumbukumbu ya mapenzi yako ya dhati, wema wako tutaukumbuka daima, tutakukumbuka daima kila tutakapolitaja jina lako, kumbukumbu zetu kwako haziwezi kuelezeka, Daima utabaki kuwa mioyoni mwetu tunakuombea upumzike kwa Amani katika maisha yako haya mapya.

Utakumbukwa daima na Baba yako Anatoly H.J. Mfinanga Mama yako Esther H. Mfinanga, wajomba, shangazi na mama wote, Mama mkwe, shemeji zako, mkeo Catherine, wanao Anatoly na Primi, Kaka zako Boniface, Bruno na Gift, dada zako Bona,Yukunda, Angela, Dorice, Luciana na Anna ndugu, jamaa na marafiki wote.

“BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”

AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...