Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (watatu kulia) akiongoza wanawake kufanya mazoezi wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo wa mpira wa pete wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Anayezuia mpira ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...