Kwa kuzingatia umuhimu wa miundombinu kuchakata na
kusafirisha gesi asilia hapa nchini, Serikali imedhamiria kuimarisha
zaidi ulinzi wa miundombinu hii.
Haya yalibainishwa mwishoni mwa
juma ambapo Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania, IGP Ernets Mangu
alifanya ziara kutembelea miundombinu ya gesi asilia kutokea
Mtwara mpaka Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, IGP aliambatana
na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dr. James Mataragio, ambapo
kwa pamoja walipata fursa ya kuona visima vinavyozalisha gesi
vilivyopo Mnazi Bay na baadae kutembelea kiwanda cha kuchakata
gesi cha Madimba na baadhi ya “Block Valve Statio-BVS” ambazo
zina matoleo kwa ajili ya kuruhusu ugawaji wa gesi asilia maeneo
ambayo yatahitaji hapo baadae.
IGP Magu aliipongeza TPDC kwa jitihada ilizofanya za ulinzi
shirikishi na kusisitiza kwamba wananchi ndio walinzi wa kwanza
wa miundombinu hii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu
akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio
pamoja na wataalamu kutoka Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Maurel
and Prom inayoendeleza gesi asilia katika kitalu cha Mnazi Bay.
Meneja Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba,
Mhandisi Kassim Mkombwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la
Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu na waliombatana nae wakati wa
ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia kutoka Mtwara hadi
Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Ernest Mangu
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu (hayuko pichani) wakati
wa ziara ya kutembelea miundombinu ya gesi asilia kuanzia Mtwara
hadi Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...