Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Andy Stephens (aliyesimama) akizungumza katika mkutano aliofanya na Wanasheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu namna nchi yake itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji wa haki nchini hasa katika maeneo ya upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na utoaji haki katika Mahakama zetu. Mazungumzo hayo yamefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyeweka mkono kichwani) akimsikiliza kwa makini Mshauri wa Makosa ya Jinai kutoka Ubalozi wa Uingereza Bw. Andy Stephens (aliyesimama) alipokuwa akizungumza kwenye kikao na Wanasheria wa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu nchi ya Uingereza itakavyoshirikiana na Tanzania katika kuboresha utoaji haki nchini hasa kwenye Mahakama za Tanzania. Kikao hicho kimefanyika leo (24/3/2016) katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...