Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali katika utoaji wa ripoti ya CEMOT  iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waliokuwa waangalizi katika uchaguzi 2015 wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Mradi-CEMOT Bwa.Bernard Kindoli akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi majimbo mbalimbali katika utoaji wa ripoti iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CEMOT,Bi.Harusi Miraji akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali wakati utoaji ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waangalizi wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
RIPOTI ya Muungano wa Asasi za Kitanzania zinazoangalia uchaguzi nchini kwa Kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CEMOT)  imesema  kuwa, kuweza kupata uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake  kwa upande wa wanawake itachukua miaka 150 kutokana na ushiriki wao kuwa mdogo katika nafasi za kugombea.

Akizungumza na waangalizi wa uchaguzi wa mradi wa CEMOT, kutoka  Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John amesema kuwa ushiriki wanawake ni mdogo katika nafasi mbalimbali za kugombea na kufanya uwakilishi wa 50 kwa 50 kuchukua muda mrefu.

Amesema kuwa wanawake waliogombea katika kiti cha urais kwa  kuchaguliwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa saba lakini hawakuweza kuingia katika  nafasi ya kwanza ya kupeperusha bendera.

Dkt.John amesema kuwa wanawake waliogombea katika nafasi ya ubunge kwa vyama vyote vilivyoshiriki  uchaguzi wa mwaka 2015 walikuwa 238 walioweza kuchaguliwa katika nafasi hiyo ni wabunge 24 tu .

Amesema kuwa ushiriki wa uchaguzi kwa wanawake ongezeko kwa mwaka 2015 ilikuwa asilimia 2 ambayo ni kiwango kidogo katika kuweza kufikia asilimia 50 kwa 50.

Ripoti hiyo  pia imesema kuwa wanawake katika nafasi ya urais ni mwanamke mmoja tu ndio aliweza kupeperusha bendera ya chama chake hali ambayo katika nafasi hiyo ni ndogo ya kufikia uwiano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wazo la 50-50 ni baya kabisa kwani litaendelea kuwakandamiza wanawake na kuwapendelea wanaume pale ambapo asilimia ya wataalam wanawake ni kubwa kuliko asilimia ya wanaume.

    Eng. UAE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...