Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini wakati alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera,kambi hiyo hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa katika makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,akizungumza na raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani), Waziri Mkuu alitembelea kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera na kuwaasa wakimbizi hao kuishi kwa kufuata sheria za nchi pasipo kuvunja amani iliyopo nchini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani),wakati ya ziara aliyoongozana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.Kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera hupokea wakimbizi kutoka nchi ya Burundi kabla ya kuwapeleka kwenye makambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,mkoani Kigoma.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...