Mbunge wa jimbo la Nyamagama,jijini Mwanza pichani akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo hilo na Mahakama kuu ya jijini Mwanza dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.
Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (CHADEMA) dhidi ya Mbunge wa sasa wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM) ilikuwa ikiendelea katika mahakama Kuu Mwanza ambapo Ezekiel Wenje alifungua kesi hiyo akipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakimpa ushindi Mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula.
Leo April 8 2016, maamuzi ya kesi hiyo yametangazwa rasmi ambapo Mbunge Stanslaus Mabula ameshinda kesi hiyo, baada ya kubainika upande wa madai hauna ushahidi unaokidhi, kuithibitishia mahakama.
Sikiliza Sauti ya Mbunge wa Nyamagana
Mh.Stanslaus Mabula akizungumza na Wanannchi mara baada ya Uamuzi wa Mahakama kutolewa leo,ambapo yeye ameibuka mshindi dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.


Wananchi wakifurahia ushindi wa Mbunge wa CCM Mh .Mh.Stanslaus Mabula.


Wananchi wakifurahia ushindi wa Mbunge wa CCM Mh .Mh.Stanslaus Mabula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...