Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo  
na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh 

Watanzania zaidi ya 1,000 mwaka huu  wanategemea kujipatia ajira kupitia kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kuanzia mwezi huu  itakapoanza kufungua vituo vidogo vya kutoa huduma zake mbalimbali muhimu vipatavyo 500 nchini kote ambako vituo 200 vitafunguliwa kati ya mwezi huu hadi mwezi Juni.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo  na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua vituo kwa kila umbali wa kilometa 10 kwenye maeneo yenye wakazi wengi kama vile kwenye miji midogo wilayani na kwenye makambi ya jeshi kwa ajili ya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguzia wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kuzipata.
Baadhi ya sehemu ambazo vituo hivyo vitafunguliwa alivitaja kuwa ni Mbaba Bay mkoani Ruvuma,Inyonga wilayani Mpanda,Pemba,Handeni,Uvinza,Karagwe,Tarime na  wilayani Chunya mkoani Mbeya.
 “Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
 Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa  vitahitaji wafanyakazi wa kuviendesha na watanzania zaidi ya 1,000 watanufaika na mpango huu .
 alizitaja baadhi ya huduma mbalimbali zitakazotolewa  katika vituo hivyo ni kuwaunganisha wateja na mtandao wa Vodacom,M-Pesa,kuuza simu, “Wateja wetu pia watapata fursa ya kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni kupitia kwenye vituo hivi”.Alisema
Alitoa wito kwa  wateja wa Vodacom  na wananchi kwa ujumla kutumia huduma hizi ili waondokane na usumbufu na kuongeza kuwa  kampuni ya Vodacom itazidi kubuni huduma mbalimbali za kuboresha maisha ya wananchi na kuwarahisishia kupata mawasiliano.

“Vodacom imedhamiria kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa teknolojia na kuwawezesha kupata mawasiliano kwa urahisi na kuanzishwa kwa huduma hii ni ushuhuda kuwa sasa huduma zake zinazidi kuwafuata wananchi popote walipo”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...