Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake. 
Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda. 
Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa 
Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.
  
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam
23 Aprili, 2015


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Pongezi nyingi sana kwa Serikali. Tumefurahi jinsi mlivyoshughulikia suala hili kwa uharaka na umakini mkubwa. Kejeri za kuwa tuko nyuma kuamua mambo zitakwisha tu. Sasa ni kazi. Wataalamu wetu hongereni sana.

    ReplyDelete
  2. Hahahaa watani wa jadi wamelamba mchanga!! Safi sana. Huyo ndo Magufuli bana

    ReplyDelete
  3. Safi sana kwa maana naona bwana mdogo Kenyata kanuna kabisa,Lazima Tz tubadilike bado ziwa Nyasa

    ReplyDelete
  4. Hakika taarifa hii imenipa furaha kupita kiwango
    This will generate employment and development of Tanga port and Tanga town and the surrounding sreas. Now the government should invest into ufufuachi wa reli ya Tanga mpaka Arusha.

    ReplyDelete
  5. Mfano huu ni wa kuigwa. Tunawashauri hata Mamlaka ya bandari PTA isikae nchi na kuanza kulalamika tuuu. Iunde jopo la wataalamu wakubaliane na TRA waondoe kodi zisizo na tija halafu waende nchi zote za jirani kueleza na kutangaza bandari zetu. Wafanye uwekezaji kweli kweli. Huu muda ni wa kufanya biashara na si kulalamika. Naamini Tanzania tungebweteka hii nafasi tusinge ipata. Bandari amkeni. Mmelala muno. Nendeni Congo, Zambia,Zimbabwe,Rwanda,na nchi nyinginezo mkajitangaze na kueleza manufaa ya kutumia bandari zetu.

    ReplyDelete
  6. The mdudu, Asante sana M7 pamoja sana hakuna tena figisu figisu hapa kazi2 huyo ndio JPM mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  7. Du! Tumelipata hata bila ya JPM kutoka nje ya nchi? Kweli hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  8. Na waweke mitego mingi ya panya.Maana nchi jirani hazita kuwa na imani ikiwa makontaina yao yakiibwa na majitu uroho

    ReplyDelete
  9. Siku zote Rais Museveni anapigania Mwl. Nyerere awe mtakatifu, unafikiri nyuma ya juhusi hizi za Rais Museveni ni nini ? . Waganda wana undugu wa kihistoria na watanzania na waganda wote wakiongozwa na Rais Museveni , Hawatosahau msaada mkubwa ulioongozwa na utu na msaada usio na masharti walioupata kutoka kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl. Nyerere . God bless Tanzania. God bless President Magufuli .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...