Hatimaye
Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari
ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.
Uamuzi
huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda
wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini
Kampala Uganda.
Ujumbe
wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji
wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa
Jopo
la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado
wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia
nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam
23 Aprili, 2015



Pongezi nyingi sana kwa Serikali. Tumefurahi jinsi mlivyoshughulikia suala hili kwa uharaka na umakini mkubwa. Kejeri za kuwa tuko nyuma kuamua mambo zitakwisha tu. Sasa ni kazi. Wataalamu wetu hongereni sana.
ReplyDeleteHahahaa watani wa jadi wamelamba mchanga!! Safi sana. Huyo ndo Magufuli bana
ReplyDeleteSafi sana kwa maana naona bwana mdogo Kenyata kanuna kabisa,Lazima Tz tubadilike bado ziwa Nyasa
ReplyDeleteHakika taarifa hii imenipa furaha kupita kiwango
ReplyDeleteThis will generate employment and development of Tanga port and Tanga town and the surrounding sreas. Now the government should invest into ufufuachi wa reli ya Tanga mpaka Arusha.
Mfano huu ni wa kuigwa. Tunawashauri hata Mamlaka ya bandari PTA isikae nchi na kuanza kulalamika tuuu. Iunde jopo la wataalamu wakubaliane na TRA waondoe kodi zisizo na tija halafu waende nchi zote za jirani kueleza na kutangaza bandari zetu. Wafanye uwekezaji kweli kweli. Huu muda ni wa kufanya biashara na si kulalamika. Naamini Tanzania tungebweteka hii nafasi tusinge ipata. Bandari amkeni. Mmelala muno. Nendeni Congo, Zambia,Zimbabwe,Rwanda,na nchi nyinginezo mkajitangaze na kueleza manufaa ya kutumia bandari zetu.
ReplyDeleteThe mdudu, Asante sana M7 pamoja sana hakuna tena figisu figisu hapa kazi2 huyo ndio JPM mpaka kieleweke
ReplyDeleteDu! Tumelipata hata bila ya JPM kutoka nje ya nchi? Kweli hapa kazi tu.
ReplyDeleteNa waweke mitego mingi ya panya.Maana nchi jirani hazita kuwa na imani ikiwa makontaina yao yakiibwa na majitu uroho
ReplyDeleteSiku zote Rais Museveni anapigania Mwl. Nyerere awe mtakatifu, unafikiri nyuma ya juhusi hizi za Rais Museveni ni nini ? . Waganda wana undugu wa kihistoria na watanzania na waganda wote wakiongozwa na Rais Museveni , Hawatosahau msaada mkubwa ulioongozwa na utu na msaada usio na masharti walioupata kutoka kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwl. Nyerere . God bless Tanzania. God bless President Magufuli .
ReplyDelete