Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake Mkoani Mwanza. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Nd, Baraka Konisaga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Nd.Biswalo Mganga.

Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe ameanza ziara ya siku tatu katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Lengo la ziara yake ni kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na zile zote zinazohusika na utoaji wa haki kwa wananchi. Taasisi atakazozitembelea ni pamoja na RITA, Ofisi ya Kanda ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Mahakama Kuu na Jeshi la Magereza.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akikabidhi Cheti cha Kuzaliwa kwa Mama wa mmoja wa watoto aliyesajiliwa katika Kituo cha Afya MakongoroJijini Mwanza. Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa katika Vituo vya Tiba inatekelezwa na RITA, Wizara ya Afya na UNICEF.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akipewa maelezo ya jinsi motto anaposajiliwa na kupata Cheti cha Kuzaliwa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembeakiangalia jinsi TEHAMA inavyotumika kutunza Kumbukumbu za Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...