Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar Ukiongozwa na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Castico (wa pili kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) baada ya mazungumzo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar Ukiongozwa na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Castico (wa pili kulia). [Picha na Ikulu.]
KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar, kesho (Aprili 23, 2016) inatarajia kukutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari Jabu imesema kikao hicho kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, iliyopo mtaa wa Kisiwandui, Mjini Unguja.
Taarifa imesema kikao hicho kawaida cha siku moja, pamoja na mambo mengine kitapokea na kujadili taarifa kadhaa kutoka Idara na Vitengo mbali mbali vya Chama hicho, ikiwemo taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar, kabla na baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar.
Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, kilichofanyika April 20, mwaka huu, chini ya M/kiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, kwa ajili ya kuandaa ajenda za kikao hicho.
Taarifa imesema kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) ya Katiba ya CCM, Toleo la mwaka 2012 na kwamba maandalizi yote yamekamilika.
Sgd.
(Waride B. Jabu),
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
22/04/2016.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...