Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman  amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya. 

Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, (katikati) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa Mahakama Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao kilichohusisha Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alipata nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika mkoa huo.

Katika kikao alichofanya na Watumishi wa Mahakama mkoani humo ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani humo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza na  Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya alipokutana nao na kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza kupunguza na kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...