Mkuu
wa Wilaya Iringa Richard Kasesela amefungua warsha ya kuwawezesha
wanafunzi kutumia kompyuta na wavuti (Bring Computer literacy to
children in Tanzania), mradi huu wa Global Out reach ulibuniwa na Bwana
Mussle ambaye alitembelea Tanzania akimtembelea binti yake aliye kuja
kijitlea Iringa (hawa ni raia wa marekani). Mradi huu unafadhiriwa na;
BENKI
KUU YA TANZANIA, ROTARY INTERNATIONAL, ROMAN CATHOLIC CHURCH IRINGA,
ST THOMAS MORE PARISH KICHANGANI, SUNRISE ROTARY USA, BRADENTON ROTARY
USA, ST STEPHENS, TTCL
Mradi huu unashirkisha shule 12 Iringa (POMELINI, MAWELEWELE,LUGALO, IRINGA GIRLS, IFUNDA TECH, NYERERE HIGH SCH, BOMALANG'OMBE,IMAGE, MAFINGA, ST JOSEPH, ST MICHAEL na CAGLIERO). Kila shule imepata kompyuta na wamepewa mafunzo, pia wametoa vifaa kwa ajili ya kituo chenye maktaba kilichotolewa kwa hisani ya baba askofu wa Roman Catholic Iringa.
Mkuu wa wilaya aliwaasa waalimu wote wa shule za sekondari kuanza kufikiria uwezekano wa kuwa na maktaba ya kompyuta. baada ya zoezi la maabara kwisha na madawati kuptakina shule zote kitakacho fuatia ni kuhakikisha shule zote zinakuwa computarized.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...