ANATOLIA KOKUSHUBILA BARONGO
1944 - 2015

Mwaka mmoja umepita tangu mama yetu mpendwa ulipoitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 15 Aprili, 2015 na kupumzishwa  Kanyigo, Misenyi-Kagera tarehe 20 Aprili, 2015.

Umetuacha katika majonzi makubwa lakini tukiwa na matumaini ya kuonana tena tukimtukuza Mungu pamoja na Malaika na Watakatifu wote Mbinguni. 

Hatutasahau upendo, ucheshi, upole, hekima, bidii yako, moyo wa kujitoa kuwahudumia wengine na kutokupenda makuu.

Unakumbukwa na Mume wako mpendwa Lambert, watoto wako Edmund, Vivien, Osbert, Comfort, Andrew na Atuganyila, wakwe zako Menrad, Justa na Mercy wajukuu zako Rehema, Mwesiga na Oleen, ndugu, marafiki na majirani.

Familia itatoa Sadaka ya shukrani katika Ibada itakayofanyika  siku ya Jumapili tarehe 17 Aprili, 2016 Saa Moja asubuhi katika Kanisa la KKKT-Tangi Bovu-Mbezi Beach.

Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, Apumzike kwa Amani,Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. You are dearly missed Mama! May our Almighty God continue to rest you in peace.

    ReplyDelete
  2. Mama mdogo tunakukumbuka sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...