Na Bashir Yakub. 

Kuvunjwa kwa mkataba ni kutotekeleza kwa matendo yale yaliyokubaliwa ndani ya mkataba/makubaliano. Hatua ya kushindwa kutekeleza makubaliano ndio kuvunjwa kwa mkataba.

 Unapomuuzia mtu kitu akalipa kiasi na kiasi akaahidi kulipa ndani ya siku saba na zikapita bila kulipa basi amevunja mkataba. Unapokubaliana na mtu kuleta bidhaa ya kiwango fulani halafu akaleta bidhaa iliyo chini ya kiwango au chini ya idadi amevunja mkataba. 

Kuvunjwa kwa mkataba kunajitokeza katika ngeli nyingi. Kwa mfano muda ni sehemu ya mkataba na hivyo jambo halitakiwi tu kutekelezwa kama lilivyoainishwa ndani ya mkataba bali pia linapaswa kutekelezwa katika muda uliokubaliwa. 

1.NAMNA MBILI ZA KUVUNJWA KWA MKATABA. 

Mkataba unaweza kuvunjwa kwa namna kuu mbili, kwa matendo au maneno. 

( a ) Kuvunjwa mkataba kwa maneno. Hii ni hatua wakati ambapo mmoja wa wahusika katika mkataba husema wazi kuwa anaachana na mkataba na hataendelea nao. Kusema kwa maneno hujumuisha hata maandishi ambapo mhusika ataandika na kusema hawezi tena kuendelea na mkataba.

 ( b ) Kuvunjwa kwa matendo. Hii ni hatua ambapo mhusika katika mkataba anavunja mkataba bila kusema wala kuandika. Matendo yake tu huashiria kuwa amevunja mkataba. Kwa mfano kutotekeleza kile kilichokubaliwa huhesabika kama kuvunja mkataba kwa matendo. Umeahidi kuleta gunia miamoja za mahindi kwa bei fulani na sasa muda umeisha na gunia ulizoleta ni 40. 

Umevunja mkataba kwa matendo. Kwahiyo kitendo cha kushindwa kutekeleza kilichokubaliwa lakini bila kesema kwa maneno/maandishi kuwa umevunja mkataba ndiko kuvunja mkataba kwa matendo( implied breach).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...