Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya uongozi Mdogo wa Polisi katika ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajent hapo chuo cha Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
Askari wa Kike wa Jeshi la Polisi ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi wakati wakimaliza mafunzo yao ya wiki nane kwenye chuo cha Polisi Ziwani.
Wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakifanya vitu vyao katika kuonyesha moja ya mafunzo waliyoyapata ya mapambano kwa singe kwenye hafla ya kumaliza mafunzo.
Askari Godrey Kihimba Mjanja akivishwa cheo cha Koplo na Balozi Seif baada kumaliza mafunzo yake na kufanya kufanikiwa kuwa miongoni mwa askari Tisa waliofanya vyema katika mafunzo yao.
Balozi Seif akimvisha cheo cha Sajenti Asha Hussein Magungu baada ya kumaliza mafunzo yake na kuwa miongozi mwa askari waliofanya vizuri katika mafunzo yao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...