Na Mwandishi Maalum, New York
Zaidi ya nchi 162 zinatarajiwa kutia saini leo ( Ijumaa) Makubaliano kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yalifikiwa jijini Paris -Ufaransa mwezi Desemba Mwaka jana.
Miongoni mwa nchi ambao zimethibitisha kushiriki hatua hiyo muhimu na ambayo ni hatua ya mwanzo kuelekeza utekelezaji wa makubaliano hayo maarufu kama Paris Agreement ni pamoja na Mataifa makubwa kiuchumi duniani na ambayo yanachangia kwa asilimia kubwa katika utoaji wa hewa ya ukaa.
Baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo katika mkutano ambao umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, nchi wanachama wa Paris Agreement watatakiwa ama kupitisha makubaliano hayo au kuridhia ( ratification).
Ili hatua ya utekelezaji ianze Nchi 55 zinatakiwa kuridhia makubaliano hayo ndani ya siku thelathini, na nchi hizo 55 zinatakiwa ziwe ni zile ambazo kwa ujumla wake zinachangia asilimia 55 ya hewa ukaa.
Taarifa kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa zimeeleza kuwa mataifa makubwa kama Marekani na China yameonyesha nia ya kutia saini makubaliano hayo huku nchi ndogo na zinazoendelea zipatazo 13 zinatarajiwa kusaini na kuridhia makubaliano hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...