Mamia ya waombolezaji, wengi wao
wakiwa wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, leo wamejitokeza kuuaga mwili wa mama mzazi wa Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Bw. Absalom Kibanda, leo
asubuhi huko Masaki jijini Dar es Salaam.
Mama yake
mzazi Kibanda, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),
ambako alikuwa akitibiwa ugonjwa wa
kiharusi. Mwili wa marehemu Marehemu Mama Gwaseko Kapyela (76) baada ya kuagwa
u mesafiriskwa kwa ndege kuelekea Tukuyu, wilayani Rungwe, mkoani Mbeya
kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi.
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam
Wanahabari nguli Neville Meena na Peter Nyanje wakiandaa shada la maua na msalaba kabla ya safari ya kwenda Tukuyu kuanza
Safari ikianza
Waombolezaji wakipeleka jeneza lenye mwili wa mama mzazi wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, baad ya hafla ya kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi ya hafla hii BOFYA HAPA







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...