![]() |
| Miss Tabata 2014 Ambasia Mallya |
MAANDALIZI ya kumsaka mrembo wa
kitongoji cha Tabata mwaka huu ‘Miss Tabata 2016’ yanatarajiwa kufanyika
kuanzia Jumanne Aprili 19 kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar es
Salaam.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga
alisema jana kuwa warembo wote waliojiandikisha wanatakiwa kufika mazoezini na
bado fomu za kushiriki shindano hilo zinaendelea kutolewa.
Kapinga alisema kwamba Keen Arts ambayo
ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment ndiyo imepewa kibali cha kuendesha
shindano hilo na waratibu wa taifa Lino Agency iliyoko chini ya mkurugenzi wake
Hashim Lundenga.Mratibu huyo alisema
uzinduzi rasmi wa shindano hilo utafanyika mwishoni mwa mwezi huu.
“Baada ya uzinduzi washiriki
watatembelea hifadhi ya Mikumi na Dar es Salaam Zoo ikiwa ni njia mojawapo ya
kutangaza utalii wa ndani,” Kapinga alisema.Aliwataka warembo wenye sifa za
kushiriki shindano hilo kujitokeza na kusema fomu hizo pia zinapatikana kwenye
ukumbi wa Da West Park na ofisi za Miss Tanzania zilizoko Mikocheni.
Miss Tabata ni miongoni mwa vituo vitatu
vilizoko kanda ya Ilala huku vingine vikiwa ni Ukonga na Dar City Centre.Washiriki watano kutoka kila kituo
watashiriki kwenye shindano la Miss Ilala na hatimaye Miss Tanzania baadaye
mwaka huu.
Ambasia Mallya ndiye mrembo
anayeshikilia taji la kitongoji hicho ambacho kimetoa wawakilishi waliofanya
vizuri katika ngazi ya taifa.Wadhamini ambao wameshathibitisha
kudhamini shindano hilo ni pamoja na CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5
na Bob Entertainment.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...