Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini akisisitiza jambo mbele ya vijana wa Kitanzania waishio New York. Zitto alipata nafasi ya kuongea na vijana hao waliotaka kujua maendeleo ya nchi yao na changamoto zake ndani ya bunge la jamhuri anavyowakilisha hoja zake kwa faida ya wananchi kupitia upinzani, pia yeye kama mwana siasa alie upande wa upinzani nini mtazamo wake juu ya kasi ya rais wa wamu ya 5.
Zitto ni mmoja ya vijana kwenye Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ni Mbunge mwenye nguvu na uwezo wa kuwakirisha hoja zenye mashiko ndani ya bunge la jamhuri na kuitikisa serikali ya chama tawala. Mfano mmoja ni suala la Escrow yeye ndiyo alikuwa chanzo cha habari hiyo iliyotikisa serikali na kupelekea wananchi kukosa imani na mwenendo mzima wa serikali ya chama tawala.
Na pia alisha wasilisha hoja ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa miezi 4. Zitto yupo New York City kwa kivuli cha World Bank na pia alipata nafasi ya kutembelea Columbia University New York na kuongea na wasomi wa huko na pia atapata nafasi ya kutembelea Harvard University huko Boston. MA. Picha na Vijimambo Blog New York.
Hapa ni Patel akiuliza swali kwa Zitto, Patel ni Mtanzania mwenye asili ya India ndiyo aliandaa mkutano huu kwa kushirikiana na Nasaan Chiume.
Zitto akipata ukodak baada ya kukutana na Watanzania New York City. Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...