Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akila kiapo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mbele ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadick mara tu baada ya kuripoti kituo chake cha kazi katikati ya wiki. Mhe. Byakanwa, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa  alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi. amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akiripoti ofisini kwake na kuanza kazi mara moja.
 Mkuu wa wilaya ya Hai mpya Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akikagua maeneo ya soko la Kwa Sadala kwa kupita kila kona na kujionea hali ya uchafu mkubwa na kuamua kuuvalia njuga.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa leo ameingia mitaani na kuanza kazi kwa kasi kwa kukagu usafi katika soko la Kwa Sadala ambako amekuta hali si nzuri na kutoa maagizo kwamba soko hilo liwe safi kila sehemu mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akifuatilia utekelezaji wa agizo lake la usafi katika soko la Kwa Sadala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...