Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiiano Profesa
Makame Mbarawa amesema Serikali
haitaongeza muda katika zoezi zima la uzimaji wa simu feki ifikapo Juni 16
mwaka huu.
Ameyasema
hayo ofisini kwake leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na kituo kimoja
cha habari hapa nchini .
Amesema
Serikali imeamua kuchukua uamuzi huo kutokana na madhara mbalimbali yatokanayo
na simu hizo ikiwemo ya kiafya na kusisitiza kuwa serikali inapoteza mapato
mengi kutokana na uingizwaji wa simu hizo nchini.
‘Tunategemea
kuzima simu zote feki kutokana na madhara yake kiafya hasa kwa watumiaji, kukosekana kwa viwango
vya ubora wa simu hizi na hivyo wananchi kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya
ununuzi wa simu hizi kwani hufa mara kwa mara’, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa ameongeza kuwa kwa sasa Jopo la wataalamu kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) limepelekwa mkoani Singida kwa ajili ya kutoa elimu
ya utambuzi wa simu hizo ili kuweza kuwasaidia wananchi kubaini kwa urahisi.
Amesisitiza
wananchi kuchukua tahadhari kabla ya kununua simu ikiwemo kumuuliza muuzaji
kabla ya kununua, kudai risiti na kuituinza ili kudhibiti uingizwaji na
usambazaji wa bidhaa hizo nchini.
Katika
hatua nyengine, Waziri Mbarawa amesema kuwa suala la mkongo wa Taifa
linaendelea vizuri ambapo Serikali kwa kushirikiana na watoa huduma wa
mawasiliano wanaendelea na usimikaji wa minara ya mawasiliano katika sehemu
mbalimbali za nchi hususan vijijini ili kuleta huduma bora za mawasiliano
nchini.
‘Kwa
sasa awamu ya nne ya mradi huu wa Mkongo wa Taifa unaendelea, kwani makampuni mbalimbali
ya simu yanasimika minara yao katika sehemu mbalimbali za nchi ili kusambaza na
kuboresha mawasiliano kwa wananchi’, amefafanua Profesa Mbarawa.
Ameongeza
kuwa uwepo wa mkongo huo nchini kumepelekea mapinduzi katika
sekta ya mawasiliano, mabenki na kuiongezea Serikali pato kwani hata nchi za
jirani hutumia mkongo huo katika kupata mawasiliano yaliyo bora.Tathmini
imebainisha kuwa kutokana na uwepo wa mkongo huo nchini watumiaji wa simu
wamefikia milioni 39.7 na wa intaneti kufukia milioni 17.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi).



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...