Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando (kushoto) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Jana , ambapo alisomewa shitaka la matumizi mabaya ya madaraka. (Picha na Maktaba).
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mkewe Eva Mhando na mtoto.
Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, hivyo kulingana na ushahidi walioutoa mahakamani, umeonyesha dhahiri kwamba hawana hatia na wameachiwa huru.Kesi yao imesomwa na Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...