Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akimkaribisha ofisini
kwake Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anawasili ofisini kwake kwa lengo la
kujitambulisha kwa Waziri huyo mara baada ya kuteuliwa na Shirika lake kuja
kuiongoza UNHCR nchini. Hata hivyo, viongozi hao katika mazungumzo yao
walijadiliana masuala mbalimbali jinsi wa kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
(kulia), akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati Mwakilishi huyo
alipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha baada
ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),
akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo
alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha
baada ya kuteuliwa na UNHCR kuja kuwa kiongozi wa Shirika hilo nchini. Wa pili
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke. Katikati ni
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo, Yoko Akasaka, na Afisa wa Shirika hilo
nchini, Daria Santoni (wa pili kulia).
Mwakilishi
Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa
Kapaya (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga wakati Mwakilishi huyo mpya nchini alipomtembelea Waziri huyo ofisini
kwake kwa lengo la kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na UNHCR kuwa
kiongozi wa Shirika hilo nchini.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi
Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa
Kapaya (katikati), pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison
Mseke. Kapaya ameteuliwa na UNHCR kuwa Mwakilishi wa Shirika hilo nchini na
amemtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, hata
hivyo katika mazungumzo yao walijadiliana masuala mbalimbali ya jinsi ya
kuwahudumia Wakimbizi waliopo nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...