Na Grace Michael
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya umetoa msaada wa saruji tani tatu katika shule
ya Sekondari ya Kilangalanga iliyopo mkoani Pwani kwa lengo la kujengea
ukuta na kuimarisha hali ya usalama shuleni hapo.
Akikabidhi
msaada huo, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani alisema
kuwa Mfuko unatoa kipaumbele kikubwa katika suala la elimu kutokana na
kuwa na umuhimu mkubwa katika suala la afya.
“Jamii
ikiwa na elimu au ikielimika hata baadhi ya magonjwa yataondoka
yenyewe...hivyo Menejimenti imeona ni vyema ikawaunga mkono katika suala
hili ili hawa watoto wawe kwenye mikono salama na mazingira safi ya
kusomea,” alisema Rehani.
Aidha
aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wanasoma kwa juhudi zote
ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano ambayo
imetoa kipaumbele kikubwa katika suala la elimu.
“Nawaombeni
sana tumieni muda wenu kwa kusoma vizuri na sio kufanya mambo ambayo
yatawapotezea muda, Rais wetu wa Awamu ya Tano anapenda kila mmoja awe
na elimu bora hivyo tumieni hii fursa ili mje kuiongoza nchi badae,”
aliwahamasisha wanafunzi hao.
Kwa
upande wa Mjumbe wa Bodi wa shule hiyo Mbwana Chombiga akizungumzia
msaada huo alisema kuwa kitendo kilichofanywa na NHIF ni cha kupigiwa
mfano kwa kuwa shule hiyo imehangaika kwa kipindi kirefu bila kupata
msaada.
“Ndugu
zangu kwa kweli sisi hatuna neno la kusema zaidi ya kuwashukuru
tu...mnaona hata wanafunzi wana furaha kweli maana wanaona sasa
mazingira yao yatakuwa bora, tunawashukuru sana na tunasema
tutashirikiana nanyi katika elimu ya wananchi kujiunga na huduma za
Mfuko,” alisema Bw. Chombiga.
Katika hatua nyingine Mfuko ulikubali ombi la shule hiyo la kuwa mlezi wa shule.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani akiwasalimia wanafunzi wa shule ya Sekondari Kilangalala Mkoani Pwani.
Sehemu ya Msaada wa Saruji tani tatu ukikabidhiwa kwa shule hiyo kwa lengo la kusaidia ujenzi wa uzio
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma Grace Michael akigawa vipeperushi vyenye ujumbe wa huduma ya Toto Afya Kadi kwa wanafunzi hao.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...