Wafanyakazi
wa NMB wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu 30 wa vyuo vikuu ambao
wamepata nafasi ya kujifunza kazi za benki katika idara mbali mbali
ndani ya benki kwa muda wa miaka miwili na baadae kupata ajira ya kudumu
Mkurungezi
Mtendaji wa NMB- Bi Ineke Bussemaker akiwakaribisha wahitimu 30 wa vyuo
vikuu vilivyo ndani nan je ya nchi. Wahitimu hao watapatiwa mafunzo kwa
kipindi cha miaka miwili kisha wataajiriwa na Benki katika vitengo
mbalimbali vilivyopo makao makuu na kwenye mtandao wa matawi yake ambayo
yamesambaa nchini kote.
Wahitimu 30 wa vyuo vikuu wakimsikiliza kwa umakini Mkurungezi Mtendaji wa NMB Bi Ineke Bussemaker
- Ni waliosomea nchini na nje ya nchi
- Kupatiwa mafunzo maalumu ya ndani ya kazi kwa kipindi cha miaka miwili
NMB
imeajiri wahitimu 30 waliosoma vyuo vikuu nchini na nje ya nchi katika
mpango wake wakukuza vipaji kwa wahitimu wa vyuo vikuu ulioanzishwa
mwaka jana. Wahitimu hao watapatiwa mafunzo ya ndani kwa kipindi cha
miaka 2 kisha wataajiriwa na Benki katika vitengo mbalimbali vilivyopo
Makao makuu na kwenye mtandao wa matawi yake ambayo yamesambaa nchini
kote.
Mkakati
mmojawapo wa NMB, ni kuunga mkono jitihada za serikali kukuza uchumi
ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa za ajira nchini hususani kwa vijana
wanaohitimu masomo ya vyuo vikuu. Awamu hii ni ya pili ya mpango huu
wakuwapatia mafunzo ya kazi ya miaka 2 wahitimu wa vyuo vikuu waliofanya
vizuri katika fani walizokuwa wanasomea kisha kuwapatia ajira.
Katika
mchakato wakuwapata wahitimu hawa kulikuwepo na waombaji wapatao 312
ambapo baada ya jopo la wataalamu kupitia maombi hayo kwa umakini
liliweza kutoa majina ya wahitimu 125 ambao walifanyiwa usahili na
tathmini katika maeneo mbalimbali. Zoezi hili lilifanyika kwa uwazi na
umakini mkubwa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kwa wenye sifa za
kuingia kwenye mpango huu kama ambavyo ilitangazwa kabla ya kuanza zoezi
la kupata waombaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa NMB – Bi Ineke Bussemaker amesema kuwa NMB ni moja ya
mwajiri mkubwa katika sekta ya benki nchini ikiwa imeajiri wafanya kazi
zaidi ya 3,000 na ikiwa inawajali wafanyakazi wake wa kuwajengea
mazingira mazuri ya kazi.
Akiongea
na waandishi wa habari, Bi Ineke Bussemaker alisema, “Nafurahi kuwa
benki yetu imekuwa kipaumbele kuwaajiri vijana hawa ambao watapatiwa
mafunzo mbalimbali kuhusiana na sekta ya kibenki katika ofisi zetu za
makao makuu na kwenye matawi yetu zaidi ya 175 ambayo yamesambaa nchi
nzima. Muhimu zaidi nina furaha kuwa kwenye uchaguzi wa zoezi hili,
tumechagua wanawake 15 na wanaume 15 bora katika kundi hili.”
Katika
kipindi cha miaka 10 tangu NMB ibinafsishwe mnamo mwaka 2005 imeongeza
ajira zaidi ya 1,500 ambapo kwa sasa inao wafanyakazi wapatao 3,140.
Benki inajivunia kujenga mazingira bora kwa wafanyakazi wake kwa kufuata
misingi ya ajira inayokubalika kitaalamu na mwaka hadi mwaka imekuwa
ikiboresha hali inayoifanya kuwa sehemu nzuri inayovutia wengi kutaka
kuwa waajiriwa wake.






Hatua ya kuwezesha wahitimu wetu wa vyuo vikuu ni nzuri ya kuigwa na waajiri wengine. Hawa vijana ukiwawezesha kuelewa kazi unaweza kukaa nao kwa muda mrefu tuwezeshe wahitimu.
ReplyDelete