Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza kuhusiana na kuaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba waliokandokando ya barabara, jijini Dar es Salaam leo. 
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa agizo la kuwaondo watu wanao ombaomba kandokando ya barabara jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa katika kuweka jiji safi itaanza na operesheni ya kuondoa ombaomba wanaokaa kandokando ya barabara kwa ajili ya kuomba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba wanakuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.

Makonda amesema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Aprili 18 mwaka huu ambapo kazi hiyo itafanywa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Amesema watu wanaofanya kazi hiyo waanze kuondoka wenyewe kutokana na mikakati waliopanga jinsi ya kutekeleza operesheni hiyo.

Makonda amesema operesheni ya kuondoa omba omba ni endelevu kutokana na kuwepo kwa uchafu kwa baadhi yao kulala katika majengo  na kufanya uchafu huo.

Nae Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa operesheni hiyo watatekeleza kuanzia siku hiyo hivyo waanze kuondoka mara moja.

Amesema agizo la Mwenyekiti wa ulinzi na usalama la Mkuu wa Mkoa kazi kwa jeshi la polisi ni kutekeleza tu  kutokana na jamii hiyo inatoka katika sehemu zenye mamlaka ambapo kuna utaratibu juu ya kuwakimu watu wenye mahitaji maalum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. omba omba wanaweza kuondoka mjini bila kuwasaka kwa nguvu bali kwa kuangalia mazingira wezeshi ya wao kubaki mjini. kwa mfano kuwepo kwa mama ntilie kila kona hapa mjini, kuwepo kwa biashara katika kial jengo mara ifikapo saa 12 jioni katikati ya jiji la dar nk . hivi visipokuwepo omba omba atakula wapi? kwa mazingira haya lazima atahamia uwanja wa fisi.

    ReplyDelete
  2. JIPU LINGINE NI WALE WATOTO WANAOOMBA SANA SANA PALE MATAA YA MOROCO NA WENGINE WANAOSAFISHA VIOO VYA GARI BILA RIDHAA.` ITAFUTWE MBINU YA KUWASAIDIA MAANA WANATAFUTA RIZIKI KWA KUFUTA VIOO LAKINI WENGINE NI VIBAKA UKIKAA HOVYO UNAKWAPULIWA NA AKISHAOSHA INAKUWA NI KAMA LAZIMA UMPE CHOCHOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...