Na  Raymond Mushumbusi MAELEZO.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaendesha mafunzo ya wiki mbili kwa Wahandisi na mafundi wa Temesa ili kuwajengea uwezo katika kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua.

Akifungua mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea uwezo wahandisi na mafundi ili kuweza kutumia teknolojia ya umeme wa nishati ya jua ambao umekuwa na tija kubwa hasa kwa sehemu ambazo umeme wa kawaida haujafika.

“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mafunzo,Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof Cathbert Kimambo amesema kwa kushirikiana na Temesa wameamua kutoa mafunzo kwa wataalamu hao juu ya teknolojia ya nishati ya umeme wa jua ili kuwasaidia kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa na utalaamu na uwezo wa kufanya kazi kulingana na mabadiliko yaliyopo.

Mmoja wa wahandisi Kutoka Temesa Bi Sara Moses ametoa wito kwa Wahandisi wengine kuwa na utaratibu wa kujifunza na kuongeza utaalamu ili kuwezesha kuendana na mabadiliko Sayansi na Teknolojia katika kuleta ufanisi katika kazi zao.
  kaimu Mtendaji Mkuu Temesa  Mhandisi Manase Ole Kujan (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya ufungaji wa moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) kutoka kwa Mhandisi Zuhura Semboji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili kwa wahandisi na mafundi wa Temesa.
  Kaimu Mtendaji Mkuu Temesa Mhandisi Manase Ole Kujan (katikati) akiangalia moja ya kifaa cha kupimia umeme kinachotumika katika mafunzo kwa wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
  Mhandisi Amani Mwanga akitoa maelekezo ya namna ya kufunga moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
 Fundi Sanifu kutoka Temesa Mganza Juma (Katikati)akiwa makini kufunga moja ya mtambo wa umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.
Baadhi ya wahandisi kutoka Temesa wakiwa katika harakati za kuchuna na kuunga nyaja katika moja ya mitambo ya umeme wa nishati ya jua (Solar) Katika mafunzo ya  wahandisi na mafundi wa Temesa yaliyofunguliwa leo.(Picha Zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...