RATIBA YA SHUGHULI ZA MSIBA WA ANDREW "404"SANGA.

Hapa Chini ni ratiba ya shughuli zinazoambatana na msiba, taarifa zilizomo ni kutoka Kamati zinazohusika na majukumu husika.

1)HARAMBEE (Leo 04/23/16)
Tutakuwa na harambee kuchangisha fedha za kusafirisha mwili na Gharama zinginezo hapo KESHO, Jumamosi kwenye ukumbi huu hapa chini kuanzia saa tisa Alasiri (1500 Masaa ya Kijeshi)

11916 Bissonett Suite #170
Houston, TX 77099

2)HUDUMA ZA KIROHO NA KUAGA MWILI (04/30/16)
Kutakuwa na Huduma za Kiroho na kuuaga mwili wa Marehemu Jumamosi IJAYO,tarehe 04/30/16 kuanzia SAA SABA MCHANA (1300 Masaa ya Kijeshi) kwenye Kanisa hili hapa chini:

CHIRST THE SERVANT LUTHERAN
CHURCH
Anwani : 2400 S. Wilcrest Dr
Houston, TX 77042
Wanajumuia tunasisitizwa kujali
Muda uliotajwa kwani ratiba itazingatiwa ili kuweza kupisha huduma zingine za Kiroho ziendelee Kanisani hapo.

***SISITIZO: Hapa ndipo patakuwa mahali pekee pa kuweza kuaga mwili wa Marehemu na kutoa heshima za mwisho.
***USHAURI: Tafadhali kwa tunaojua hatotoweza kuhimili hisia zetu tunao uamuzi wa kutoshiriki tendo hili. Tuamue kwa busara zetu kadri dhamira zetu zitakavyotutuma.

3)KUSHEREHEKEA MAISHA YA ANDREW: (30/04/16)
Wanajumuia wameona ni vyema kusherehekea maisha ya Andrew kwa kukutana na kujifariji pamoja kuanzia saa 12 jioni.
Tutakutana Jumamosi baada ya Kuuaga Mwili kanisani kwenye ukumbi wa Harambee kwa Misa Maalumu itakayofuatiwa na chakula cha pamoja tukisherehekea maisha yetu na Andrew kwa pamoja.

Sienna Hall
11916 Bissonett Suite #170
Houston, TX 77099.

Kny Kamati ya Mazishi
Saidi Nusura, Katibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...