Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam imetoa shilingi milioni 19.5 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya akina mama na vijana wajasiriamali katika Manispaa hiyo ili kuwasaidia kujikwamua kibiashara.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukabidhi hundi kwa vikundi hivyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob alisema kuwa fedha hizo zinatokana na asilimia kumi ya mapato ya halmashauri ambayo hutengwa kila mwaka.
“ Ndugu zangu Mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ilitenga shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya kuviwezesha vikundi na fedha bado ipo kwa wale wanaohitaji wajiunge waje wachukue
"Na Mwaka wa fedha 2016/2017 tunatarajia kutenga kiasi cha shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wakina mama kwenye halmashauri yetu.”alisema Mstahiki Meya.
Naye Meneja wa vikundi kutoka Benki ya Wananchi wa Dar es salaa (DCB Plc) Benki ambayo huhifadhi fedha hizo na kuzitoa kwenye vikundi vya ujasiliamari, Bi Maria Kabeo alisema Benki hiyo ipo tayari kutoa fedha kwenye kikundi ambacho kitahitaji na kukidhi vigezo
Amewaasa vijana kujiunga vikundi vya watu watano na kuchangamkia fursa hiyo.
Vikundi vilivyonufaika na msaada huo ni kikundi cha Kigogo Mbuyuni kata ya Kigogo ambacho kinafanya shughuli za mama lishe,ushonaji na Saloon,ambapo kimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 7.7.
Kikundi cha Kilungule B kata ya Saranga kimepatiwa kiasi cgha shilingi milioni 3.
Vikundi vingine ni kikundi cha Live Skills Stop over (LISEDO) ambacho kimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 2.1,na kikundi cha Saranga B ambacho kimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 4.1 pamoja na kikundi cha Goba Kinzudi kata ya Goba ambacho kimepatiw3a kiasi cha shilingi milioni 2.65.
Wenyeviti wa vikundi hivyo kwa nyakati tofauti wamemshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo pamoja na Benki ya DCB Plc kwa hatu waliyoifanya nakuwaomba waendlee kutoa miko hiyo kwa riba nafuu kama ilivyo sasa ambapo tozo ya riba ni asilimia kumi.
“Mh.Meya tunashukuru sana,na sisi tunafarijika kwa kutuunga mkono tutazitumia pesa hizi kwa malengo ambayo tumejiwekea kama kikundi,na tunawaomba vijana wajitokeze kujiunga na vikundi ili wajikwamue kimaisha”alisema Semeni Mahita mwenyekiti wa kikundi cha Kigogo Mbuyuni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob akikabidhi hundi ya mfano kwa Diwani wa Saranga Stop Over, Ephraim Kinyato kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya akina mama na vijana wajasiriamali jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob akikabidhi hundi ya mfano kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya akina mama na vijana wajasiriamali Saranga Kimara B
Mkuu wa idara ya Jamii wa Manispaa ya Kinondoni Bi. Mwajuma Magniza akitoa elimu kwa wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo.
Akina mama na vijana wajasiriamali wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...