Kikosi cha Simba Ughaibuni Marekani.
Kikosi cha Yanga Ughaibuni Marekani
 
Aliyekuwa mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lilly Munanka akisalimiana na wachezaji wa Yanga ambao ndio walichukua kombe la DICOTA mwaka 2011 ilipofanyika Washington, DC.
Aliyekuwa mkuu wa utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lilly Munanka akisalimiana na wachezaji wa Simba.



Siku ya Jumamosi April 30, 2016 itakua historia kujiludia pale mpambano wa Simba na Yanga za Ughaibuni Marekani utakapoandika ukurasa mpya kwa mara ya kwanza kuchezewa Dallas, Texas.
Mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki watakaohudhuria kongamano la DICOTA kutoka Tanzania wakiwemo watakaotoka majimbo mbalimbali Marekani, ni mpambano utakaoandika historia mpya
Mpambano huo utakaoenda sambamba na nyama choma ikiwemo michezo ya watoto, mpira wa kikapu na mpira wa wavu, unatarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Huffhines Recreation Center anuani 200 N Piano Road, Richardson, TX 75081 na mechi inatarajiwa kuanza saa 10 jioni (4pm).
Habari za uhakika zilizotufikia ni kwamba tayari kamati za ufunzi za timu hizo zimeshawasili kutoka Bongo na maandalizi ya kuweka mazingara bora yapo katika hatua za mwisho. Kamati ya Yanga inatoka Wete, Pemba, wakati kamati ya Simba inatoka Mlingotini wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani
Mechi ya Simba na Yanga Ughaibuni Marekani itakuwa wazi kwa kila shabiki kucheza na kila shabiki kushangilia. Mpambano wa Simba na Yanga uliofanyika Washington, DC Octoba 16, 2011 Yanga iliibuka mshindi wa kombe hilo la DICOTA baada ya kuibamiza Simba kwa bao 6-4 baada ya dakika 90 timu hizo kufangana bao 4-4 na kuongezwa muda wa nyongeza dakika 15 kila kipindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...