Siku ya Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry unatarajiwa kusafirishwa jioni ya leo kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.
Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake
Mr.& Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani
Waombolezaji
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani .



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...