Kamera ya Globu ya Jamii, wikiendi hii ilizuru katika Ufukwe wa Kawe Bichi Jijini Dar na kubahatika kuzinasa taswira hizi mwanana kabisa.

Samaki wakiparwa mara baada ya kutoka kuvuliwa, ambapo kila ifikapo Jioni huwa kunakuwa na Mnada wa Samaki katika ufukwe huu wa Kawe.
Mdau akila Tizi Ufukweni.
Muonekani kwa upande mwingine wa Ufukwe.
Chombo kikirejea.
Chombo kimepaki baada ya safari ndefu ya Baharini katika Uvuvi.
Mdau akitabaruku ufukweni.











Kiongozi ungetia neno kuhusu uchafu huo uliotamalaki hapo, uchafu huo umaharibu mandhari yote ya fukwe!!!
ReplyDeleteWabongo tunatia aibu! ufukweni mbona kuchafu hivyo????
ReplyDeleteHizi ni taswira za uchafuzi wa mazingira na sio mwanana. Fukwe zinahitaji usafi wa kila siku.
ReplyDeletePwani nzuri ila huo UCHAFU! Mifuko ya nailoni inachafua sana mazingira.
ReplyDeleteUfukwe mchafu hivi kunawahusika au inabidi kutoza pesa ili kuajiri wasafisha fukwe. Athari kwa viumbe majini inaweza kuwepo hasa kutupa plastiki. Wahusika wasafishe fukwe.
ReplyDeleteUfukwe mzuri, ila ni bora wahusika wasimamie usafi wa mara kwa mara
ReplyDeleteHuo uchafu wote ufukweni. Kweli tubadilike Kama anavotuasa Rais Magufuli. Ufukwe gani huo?
ReplyDelete