Na Woinde Shizza,Karatu

Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.

Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.

Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua zozote ambazo wamezichukuwa.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.

Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye amechukuwa hatua .

“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja na kutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada ya kutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizo lililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katika kituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezi kuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyaje unakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache ale akitosheka aondoke “alisema Seuri lazier

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tatizo ni sisi binaadamu kwenda kuweka makaazi yetu kwenye ardhi ya wanyama hao.sisi binaadamu siku zote tunaona wanyama hawana haki lakini wanyama wanaijua haki yao na wanaijua ardhi waliorithi kutoka kwa mabibi na mababu zao licha ya sisi binaadamu kujifanya hiyo ardhi ni mali yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...