Na Woinde Shizza,Karatu
Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya
Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.
Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa
Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti
ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.
Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka
katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na
wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua
zozote ambazo wamezichukuwa.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema
kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo
wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo
inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.
Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo
ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye
amechukuwa hatua .
“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja na
kutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada ya
kutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizo
lililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katika
kituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezi
kuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyaje
unakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache ale
akitosheka aondoke “alisema Seuri lazier
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA


Tatizo ni sisi binaadamu kwenda kuweka makaazi yetu kwenye ardhi ya wanyama hao.sisi binaadamu siku zote tunaona wanyama hawana haki lakini wanyama wanaijua haki yao na wanaijua ardhi waliorithi kutoka kwa mabibi na mababu zao licha ya sisi binaadamu kujifanya hiyo ardhi ni mali yetu.
ReplyDelete