Na Bashir Yakub. 

Wapo baadhi ya askari hutumia nafasi zao vibaya. Wapo wanaojua na kutekeleza wajibu wao wa kisheria na wapo wasiotekeleza wajibu wao wa kisheria. Raia hulalamika sana. 

Moja ya maeneo makubwa yanayolalamikiwa ni hili la kukamatwa bila sababu za msingi/kuwekwa ndani bila sababu za msingi na wakati mwingine kufunguliwa mashtaka bila sababu za msingi. 

Leo sio ajabu askari kugombea mwanamke na mwanaume mwenzake halafu akamtafutia sababu na kumweka ndani au akambambika shitaka bila kosa lolote. Leo sio ajabu kutupiana maneno mawili matatu na askari halafu ghafla ukaambiwa umekamatwa na bunduki, leo sio ajabu mwenye hela kuamua amfunge nani kwa kutumia askari . Matukio ni mengi yanayofanana na haya.

 1.KUENDELEA KWA MATENDO YA KUKAMATWA/KUWEKWA NDANI BILA SABABU ZA MSINGI. 

Hakuna shaka matendo haya yameendelea kwasababu wanaotendewa huwa hawachukui hatua. Mtu anakamatwa anawekwa ndani bila sababu za msingi akiachiwa anashukuru na kuondoka. Mwingine anabambikiwa kesi inamtesa miaka na miaka ikiisha anashukuru na kuondoka. 

 Namna hii haiwezi kuwa suluhu. Kama hii itakuwa suluhu basi wengi wajiandae kuumia. Makala yanazungumzia kukamata au kuweka ndani bila sababu za msingi( false imprisonment/arrest). Hii isichanganywe na kumshitaki mtu bila sababu za msingi( malicious prosecution). Japo kwa namna fulani yanafanana lakini makala haizungumzii kushitaki bila sababu za msingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...