
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhe George Simbachawene akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda nyaraka za jengo la Machinga Complex (pichani juu) baada ya kuvunja bodi ya jengo hilo mapema leo kwa kushindwa kazi, na kutangaza kuwa amelikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa leo jijini Dar es Salaam. Jengo hilo lilijengwa mahususi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) ili kuwaondoa mabarabarani na kupunguza msongamano wa Wamachinga mitaani, lengo ambalo Bodi iliyovunjwa imeelezwa kuwa ilishindwa kutimiza.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...