Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, aliwasili nchini jana usiku pamoja na Ujumbe wake kwa lengo la kushiriki Kikao cha Kujadili Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao hicho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia ) akizungumza na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni (kushoto) mara baada ya Waziri huyo pamoja na ujumbe wake kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kulia) akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya ujenzi wa mabomba kutoka Uganda, Habumugisha Johnbosco (kushoto) aliyeambatana na ujumbe wa Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati- Petroli, Erasto Simon (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...