Mbunge wa jimbo la Mafinga mkoani Iringa Bw Cosato Chumi (kulia) akimpongeza wakili wake Asheri Utamwa baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kutoa hukumu iliyompa ushindi mbunge Chumi kufuatia kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kupitia Chadema Bw Willy Mungai.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi akiweka sawa bendera ya ubunge leo kabla ya kuondoka viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya kushinda kesi ya uchaguzi ,kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama katibu mtoto nchini Tanzania.
Wakili maarufu wa Chumi Bw. Asheri Utamwa (kushoto ) akizungumza na wanahabari baada ya mteja wake Chumi kulia kushinda kesi ya uchaguzi leo.

Na fredy mgunda,Iringa.
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimempongeza mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi baada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Willy Mungai .

Akizungumza na wanahabari leo nje ya viwanja wa mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya mahakama kutoa huhukumu iliyompa ushindi Bw Chumi ,katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama alisema kuwa baada ya hukumu hiyo ya mahakma kumpa haki mbunge huyo wa CCM kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni kuona utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa kwa nguvu zote.

“Hapa kwa hukumu hii haki imeweza kutendeka kwani kabla ya kutoa hukumu jaji alisoma na kutolea ufafanuzi wa vipengele vyote ambavyo mlalamikaji alikuwa anavilalamikia na baada ya hapo ndipo alipoweza kutoa hukumu ya kesi hiyo “

Hata hivyo alisema pamoja na hukumu hiyo kutolewa bado wanachama wa Chadema na wale wa CCM katika jimbo la Mafinga hawana budi kuendelea kuwa wamoja ili kushikamana na mbunge wao kuleta maendeleo jimboni .

Kwani alisema suala hilo la kesi mahakamani mbali ya kuchelewesha majukumu ya mbunge kwa wananchi wake bungeni bado lilikuwa likimfanya mbunge muda wote kuwa ni mtu wa kuwaza kesi badala ya kuwaza namna gani ya kuwatumikia wananchi wake.

“ Ninawaomba wenzetu Chadema wasifikilie kukata rufaa kuendelea na kesi hiyo kwani katika hoja zao zilizopelekea kwenda mahakamani ufafanuzi umetolewa vizuri na jaji hivyo kuendelea kukata rufaa ni kuendelea kuwacheleweshea wananchi wa jimbo la Mafinga kupata maendeleo “

Pia alimtaka mbunge huyo Bw Chumi kufidia muda ambao ameupoteza kwa kushinda mahakama kusaka haki kwa kwenda kuwatumikia wananchi wake kwa kasi ya hapa kazi tu ili jimbo hilo lizidi kusonga mbele kwa maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge Chumi alisema anapenda kuwashukuru wananchi wake wa jimbo la Mafinga ambao walitoa ushirikiano kwa kufika mahakamani kutoa ushahidi muda wote na kuwa zaidi anamshukuru mwenyezi Mungu kwa kusimamia haki katika kesi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...